Eneo ambalo inategemewa kujengwa Ofisi ya Tume ya Pamoja ya Fedha – Zanzibar katika mji wa Serikali uliopo Kisakasaka, Mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Magharibi B, Zanzibar.
Katibu Msaidizi Ofisi ya Tume Zanzibar Bw. Haji K. Haji (wa kwanza kulia) akimuonesha Katibu wa Tume (wapili kulia) na Wajumbe wa Menejimenti (baadhi hawapo pichani) mipaka ya eneo ambalo inategemewa kujengwa Ofisi ya Tume Zanzibar katika mji wa Serikali uliopo Kisakasaka, Mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Magharibi B, Zanzibar.
Wajumbe wa Menejimenti ya Tume wakiwa katika Kikao Kazi cha Menejimenti kilichofanyika kuanzia tarehe 06 – 08 Oktoba, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Tume Zanzibar
Katibu wa Tume ya Pamoja ya Fedha, Bw. Ernest M. Mchanga (watatu kulia), Katibu Msaidizi Ofisi ya Tume Zanzibar Bw. Haji K. Haji (watatu kushoto) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Menejimenti ya Tume na baadhi ya Watumishi wa Ofisi ya Tume Zanzibar baada ya Kikao Kazi cha Menejimenti kilichofanyika kuanzia tarehe 06 – 08 Oktoba, 2025